BETI NASI UTAJIRIKE

SVEN AUZUNGUMZIA MCHEZO WA FAINALI DHIDI YA NAMUNGO



Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kuwa anakutana na timu bora kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Agosti 2, Uwanja wa Nelson Mandela,  Sumbawanga. 
Utatu wa Namungo una jumla ya mabao 27, ukiongozwa na Relliants Lusajo mwenye mabao 12, Bigirimama Blaise mwenye mabao 11 na Lukas Kikoti mwenye mabao manne.

Mbelgiji wa huyo amesema kuwa mchezo huo hautakuwa mwepesi kwa kuwa wanakutana na timu ambayo ina wachezaji wazuri kuanzia safu ya ushambuliaji pamoja na viungo wazuri.

"Timu yetu inapewa nafasi kubwa ya kushinda kwenye fainali ya FA dhidi ya Namungo kutokana na ubora tulionao lakini kwa upande wangu natarajia kuwa mchezo huu utakuwa mgumu.

"Wana safu ya kiungo iliyo bora na kuna wale washambuliaji wazuri ambao ni hatari ikiwa ni Lusajo na Blaise hatupaswi kuwapa nafasi hata kidogo,".

Namungo ilitinga hatua hiyo kwa kushinda bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars na Simba ilishinda mabao 4-1 mbele ya Yanga Uwanja wa Taifa.

Post a Comment

0 Comments