BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA YAIDHARIRISHA VIBAYA YANGA LIGI KUU SERENGETI


Simba Queens imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya wapinzani wake Yanga Princess kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili  Simba ilipata mabao hayo kupitia kwa Mwanahamisi Omary dakika ya 32 na 75, Oppah Clement akifunga dakika ya 65 na 82 ambao walifunga mabao mawili mawili huku bao jingine likifungwa na Joelle Bukuru dakika ya 69.

Joel Nasri dakika ya 35 alipachika bao pekee la Yanga Princess ambayo imepanda ligi msimu uliopita ikiwa  haijabahatika kupata ushindi mbele ya Simba.Timu hizo zimekutana mara nne huku Simba Queens ikifunga jumla ya mabao 20 na Yanga Princess ikifunga jumla ya mabao matatu.

Post a Comment

0 Comments