BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA WAPO TAYARI KUIVAA NAMUNGO FC


Kikosi cha Simba kimeondoka leo Alhamisi Julai 30 mjini Mbeya kuelekea mkoani Rukwa tayari kwa mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Namungo utakaopigwa Jumapili. Baada ya maandalizi ya kambi ya siku tatu kikosi kiko tayari kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali ambao utapigwa katika Uwanja wa Nelson Mandela. Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck amesema kikosi kipo kamili wachezaji wako kwenye hali nzuri na morali ipo juu tayari kwa mchezo. Sven amesema lengo lililobaki kwa sasa ni kuhakikisha tunachukua taji la pili msimu huu baada ya kunyakua ubingwa wa ligi wiki chache zilizopita

Post a Comment

0 Comments