BETI NASI UTAJIRIKE

RUVU SHOOTING NA LIPULI WAZIDI KUFANYA MAMBO MAZURI VPL


Ruvu Shooting  imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.Mabao ya Ruvu Shooting katika mchezo wa leo yamefungwa na Santos Mazengo dakika ya 39 na 90 na Saadat Mohamed , wakati ya Mwadui FC yamefungwa na Enock Jiah dakika ya tisa na Wallace Kiango dakka ya 56.

Kwa ushindi huo, Ruvu Shooting inafikisha pointi 47 baada ya kucheza mechi 35 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya nane, sasa ikizidiwa pointi moja na JKT Tanzania inayoshika nafasi ya saba, wakati Mwadui FC inashuka kwa nafasi moja hadi ya saba ikibaki na pointi zake 40 za mechi 35.


Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, bao pekee la Erick Msagat dakika ya 50 limetosha kuipa Polisi Tanzania ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Biashara United Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.

Ushindi huo unaifanya Polisi ifikishe pointi 51 baada ya kucheza mechi 35 na kupanda kwa nafasi mpja hadi ya sita, wakati Biashara United inabaki nafasi ya 10 na pointi zake 46 za mechi 35.


Uwanja wa Samora, Iringa mabao ya Rashid Mohamed dakika ya 55 na Paul Materazz dakika ya 62 yakatosha kuipa Lipuli FC ushindi wa 2-0 dhidi ya KMC katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo. 


Lipuli sasa inafikisha pointi 40 baada ya kucheza mechi 35 na kujiinua kutoka nafasi ya 17 hadi ya 13, wakati KMC inabaki nafasi ya 12 na pointi zake 43 za mechi 35.

Post a Comment

0 Comments