BETI NASI UTAJIRIKE

REAL MADRID WANAHITAJI POINTI 1 TU WATANGAZWE MABINGWA LA LIGA


Klabu ya Real Madrid imeendelea kufanya vyema ligi kuu Hispania -La Liga baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Granada. Ferland Mendy alikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 10 ya mchezo huku Karim Benzema akifunga bao la pili dakika ya 16 na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika kwa Real Madrid wakiongoza kwa mabao 2-0.

Darwin Machis aliipa Granada bao la kufutia machozi dakika 50 ya mchezo na kufanya matokeo kuwa ni 2-1 mpaka mwisho wa mchezo.Kwa matokeo hayo Real Madrid anaendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi akiwa na pointi 83 kwenye michezo 36 aliyocheza. 

Real Madrid anahitaji pointi 1 tu kwenye michezo miwili iliyobaki. mchezo wa kwanza ni ule dhidi ya Villareal na Leganes kama atashida au kusuluhu mchezo mmoja kati ya hiyo basi atatangazwa kuwa bingwa mpya la Liga msimu wa 2019/20

Post a Comment

0 Comments