BETI NASI UTAJIRIKE

RASMI : REAL MADRID MABINGWA WAPYA LA LIGA MSIMU WA 2019/20


Klabu ya Real Madrid imefanikiwa kutwaa ubingwa wa La Liga mimu wa 2019/20. Real Madrid wametwaa kombe hilo baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Villareal.Shukrani za kipekee zimwendee Karim Benzema aliyefunga mabao yote mawili dakika ya 29 na penati maridhawa dakika ya 77 na kufanya Real Madrid kufikisha pointi 86 kwenye msimamo wa ligi wakicheza michezo 37. Nafasi ya pili inashikiliwa na Barcelona wenye pointi 79.

Real madrid imetwaa kombe hilo kwa mara ya 34 na kuwafanya waendelee kuongoza kwa idadi kubwa ya makombe ya La Liga na nafasi ya pili inashikiliwa na Barcelona yenye makombe 26.

Karim Benzema anaongoza orodha ya ufungaji kwa wachezaji wa Real Madrid akifunga mabao 21 huku nafasi ya pili ikishikiliwa na beki mkongwe Sergio Ramos. Timu hiyo imebakiwa na mchezo mmoja dhidi ya Leganes ambao watakabidhiwa kombe mara baada ya mechi hiyo.

Post a Comment

0 Comments