BETI NASI UTAJIRIKE

PICHA : FEISAL SALUM AKABIDHIWA TUZO YAKE NA SPORT PESA


Kiungo mchezeshaji wa klabu ya Yanga Feisal Salum amekabidhiwa rasmi tuzo ya mchezaji bora kwa klabu ya Yanga na wadhamini wa klabu hiyo kampuni ya SportPesa.Feisal alipigiwa kura na mashabiki wa Yanga na kuibuka mshindi.

Mchezaji huyo amekabidhiwa hundi yenye thamani ya milioni 1 pamoja na tuzo maalumu.Msemji wa klabu hiyo Antonio Nugaz alishiriki tukio la utolewaji wa tuzo hizo zilizokabidhiwa na mkurugenzi wa SportPesa nchini Bw.Tarimba .Feisal aliandika " Sina Budi kumshukuru mwenyezi Mungu na pia sina budi kuwashukuru wanayanga wote kwa kunipigia kura viongozi wangu wa Yanga  nawapenda sana mashabiki wa Yanga asanten sana mashabiki wangu nawapenda sana

Naye msemaji wa Yanga Antonio Nugaz aliandika Kongole kwako @feisal194 kwa kushinda tunzo ya mchezaji bora wa msimu wa Sportpesa wa mwaka 2019/20 wa Yanga 

Post a Comment

0 Comments