BETI NASI UTAJIRIKE

OKWI ANAREJEA MSIMBAZI NINI MAONI YAKO MWANA SIMBAEmanuel Okwi inaelezwa kuwa yupo njiani kurejea ndani ya Klabu ya Simba ambayo aliitumikia msimu wa 2018/19 wakati wakitwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.
Okwi amekuwa na mahusiano mazuri na Kagere ndani ya Simba pamoja na wachezaji wengine ikiwa ni pamoja na Clatous Chama ambaye ni kiungo kipenzi cha mashabiki wa Simba.

Habari kutoka ndani zinaeleza kuwa tayari mchezaji huyo amekubali kurejea ndani ya Simba ili kuendelea kufanya kazi aliyoimaliza msimu wa 2018/19 wakati alipoibukia nchini Misri.

Raia huyo wa Uganda ambaye anavaa jezi namba 7 hata kwenye timu ya Taifa ya Uganda mgongoni kwa sasa anaitumikia Klabu ya Al Ittihad ya Misri.

"Yupo njiani kurejea ndani ya Simba na kila kitu kipo sawa ni suala la kusubiri tu mambo yakamilike ili atue tena Simba," ilieleza taarifa hiyo.

Hivi karibuni Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa alisema kuwa mpango wa kusajili unategemea ripoti ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck.

Post a Comment

0 Comments