BETI NASI UTAJIRIKE

NAMUNGO WANAMSUBIRI SIMBA AU YANGA FAINALI


Namungo FC imekata tiketi ya kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Sahare All Stars Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki wa kushoto Edward Charles Manyama aliyemalizia mpira uliotemwa na kipa Fikirini Bakari kufuatia kona ya Abeid Amaan kutoka upande wa kulia.


Sasa Namungo itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili itakayopigwa kesho Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga.

Post a Comment

0 Comments