BETI NASI UTAJIRIKE

MWAKALEBELA AFUNGUKA SAKATA LA MORRISON NA YANGA


Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa suala la mchezaji wao Bernard Morrison kutokuwa na timu kwa sasa kambini huku akionekana akicheza mechi za mchangani linashughulikiwa.
Morrison raia wa Ghana amekuwa kwenye mvutano mkubwa na Klabu ya Yanga kuhusu suala la mkataba wake ambapo yeye anadai kwamba mkataba wake ni wa miezi sita na umemalizika huku Yanga ikieleza kuwa ana mkataba wa miaka miwili.
Julai 12 ilikuwa ni mara ya mwisho kwa Morrison mwenye mabao matano na pasi tatu za mabao kuonekana na Yanga ilikuwa ni kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba wakati Yanga inapoteza kwa kufungwa mabao 4-1.
 Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa nyota huyo hajaripoti kambini huku suala lake likifuatiliwa kwa ukaribu.
“Morrison ni mchezaji wa Yanga hilo lipo wazi kwa kuwa kwa sasa inaonakena anaonekana akicheza mtaani suala hilo linafuatiliwa kwa ukaribu kwani kuna sheria za kazi hivyo namna ambavyo zitaeleza hatua juu yake itachukuliwa,” alisema Mwakalebela.
  

Post a Comment

0 Comments