BETI NASI UTAJIRIKE

MWADUI FC YAJIPANGA KUIFUNGA YANGA LIGI KUU


Klabu ya Mwadui FC imesema kuwa inahitaji pointi tatu mbele ya Yanga watakapokutana leo Uwanja wa Taifa. Mwadui FC imetoka kupokea kichapo cha mabao 3-2 mbele ya Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini. 

Timu hiyo Inakutana na Yanga iliyotoka kushinda mabao 3-1 mbele ya Singida United huku ikilinda kwa nguvu zote nafasi ya . 2

meneja wa Mwadui FC Daudi Chakala amesema kuwa malengo makubwa ya timu yao ni kubaki ndani ya ligi na njia itakayowabakisha ni kushinda.

"Ili timu ibaki ndani ya ligi ni lazima ipate matokeo mazuri na hilo linawezekana kwa kuwa morali ya wachezaji ni kubwa na kila mchezaji anahitaji matokeo. 

"Mashabiki watupe sapoti ili tuweze kufikia malengo ambayo tumejiwekea, hatutaki kucheza playoff tena,"

Mwadui FC ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 40 baada ya kucheza mechi 35 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya pili ikiwa na pointi 67.

Post a Comment

0 Comments