BETI NASI UTAJIRIKE

MTIBWA SUGAR YAENDELEA KUKALIA KUTI KAVU BAADA YA SARE NA YANGA


Klabu ya Mtibwa Sugar  imejikuta kwenye hali mbaya baada ya kushindwa kuifunga klabu ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro baada ya timu hizo kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Haruna Chanongo alianza kufunga bao dakika ya 28 ila lilishindwa kuwapa pointi tatu mbele ya Yanga baada ya Adeyum Saleh kusawazisha bao hilo dakika ya 83.

Mchezo wa leo ulikuwa ni muhimu kwa Mtibwa Sugar kujiondoa kwenye hatari ya kushuka daraja huku kwa Yanga ikiwa ni kwenye kuwaongezea ufalme nafasi ya pili.

Sare hiyo inawafanya Mtibwa Sugar na Yanga wagawane pointi mojamoja.

Yanga inafikisha pointi 69 ikiwa nafasi ya pili huku Mtibwa Sugar wakifikisha pointi 42 nafasi ya 14 ambayo bado sio salama kwao kwa kuwa inaweza kufikiwa na Mbao FC yenye pointi 42 ikiwa itashinda mchezo wake wa mwisho.

Vita ya kushuka daraja inazidi kupamba moto huku Singida United ikitazama namna mambo yanavyokweda na kwenye mchezo wake wa leo imepoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Kagera Sugar

Post a Comment

0 Comments