BETI NASI UTAJIRIKE

MTIBWA SUGAR WAFUNGUKA WALIVYOICHAPA AZAM


Klabu ya Mtibwa Sugar imesema kuwa sababu kubwa iliyowapa ushindi mbele ya Azam FC ni kujituma kwa wachezaji wake ndani ya uwanja muda wote bila kuchoka.Azam FC inayonolewa na Aristica Cioaba ilikubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar inayonolewa na Zuber Katwila.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Gairo, Morogoro ulikuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa Mtibwa Sugar inapambana isishuke daraja huku Azam FC ikipambana kupambana kushinda ili kumaliza nafasi ya pili.

Katwila amesema:"Tulipoteza mchezo wetu uliopita mbele ya Mbao FC haina maana kwamba hatukuwa na uwezo hapana, wachezaji wanatambua kazi yao na wameonyesha juhudi mwanzo mwisho hivyo ndio tumeweza kupata ushindi.

"Bado tunapambana kujitoa hapa tulipo kwani mambo mengi yapo na ushindani ni mkubwa ila tunaamini kwamba tutaendelea kupata matokeo."

Ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 41 huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu na pointi 65 zote zikiwa zimecheza mechi 35.

Post a Comment

0 Comments