BETI NASI UTAJIRIKE

MSEMAJI WA AZAM FC AGEUKA MBOGO KWA HAJI MANARA


Msemaji wa Azam FC Thabit Zakaria(Zakazakazi) amemjia juu msemaji wa Simba Haji Manara baada ya kusema Azam FC ni timu kubwa lakini ni dhaifu kwa Simba kwani imefungwa miaka mitatu mfululizo na hata msimu huu imefungwa mara tano kwenye michuano mbalimbali walizokutana .Haji akalaumu kitendo cha Azam kumleta msemaji Zakazakazi kwenye klabu hiyo kwani ni mtu wa mtaani tu  na kauli hiyo ikamfanya Zakazi kumjia juu Manara

Zakazakazi kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika "Nianze na hili la mtaani. Mimi sijatoka mtaani aisee, nimetoka kwenye chombo kikubwa sana cha habari hapa nchini...hata kabla ya hapo nilikuwa kwenye chombo kikubwa sana.

Maisha yangu ya habari nimeyaishi kwenye vyombo vikubwa nikifanya kazi na magwiji wa habari.Wewe ndiyo umetoka mtaani baada ya kutoka jela na kesi yako ya utapeli.

Matapeli wote ni watu wa mtaani na ndiko wewe ulikotoka hadi Simba kukuokota.
Halafu suala la AC na dawa ndilo la kushangaza zaidi.iliandika kwamba SAFARI IJAYO HATUTOWASHA AC.

Hakuna sehemu niliyotaja dawa...nashangaa unakurupuka na hoja za dawa. Yawezekana kuna kitu unajua kuhusu dawa, utusaidie.

Post a Comment

0 Comments