BETI NASI UTAJIRIKE

MOURINHO ABANWA MBAVU TOTTENHAM IKIPIGWA


Kocha wa Tottenham Jose Mouringo ameendelea kuwa na wakati mgumu ndani ya klabu hiyo tagu alipojiunga katikati ya msimu huu. Hapo jana usiku amekubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Shiffield United mchezo uliopigwa Bramall lane.

Sheffield United wamepata ushindi wa kwanza tangu kurejea kwa Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa Tottenham Hotspur. Mabao ya Sheffield United yamefungwa na Sander Berge dakika ya 31, Lys Mousset dakika ya 69 na Oliver McBurnie dakika ya 84, wakati la Spurs limefungwa na Harry Kane dakika ya 90

Mourinho ameiongoza spurs kwenye michezo 18 michuano mbalimbali akishinda 13 sare 3 na kufungwa 2 hivyo kujikusanyia pointi 42 tangu atue klabuni hapo

Kwa matokeo hayo Tottenham inasalia nafasi ya 9 ikiwa na pointi 45 kwnye michezo 32 waliyocheza. 

Post a Comment

0 Comments