BETI NASI UTAJIRIKE

MORRISON NI JIPU NDANI YA YANGA ,AZIDI KUWA KERO KWA TIMU


Bernard Morrison ametoroka kambini jana wakati wachezaji walipokuwa wakijiaandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Kagera Sugar.Kwenye mchezo huo Morrison hakuwa sehemu ya mchezo ambapo Yanga iliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Morrison amekuwa kwenye mvutano mkubwa na uongozi wa Yanga kwa sasa ambapo ishu kubwa inaeelezwa kuwa ni kuhusu mkataba wake ambao kila mmoja anasema jambo lake.

Uongozi wa Yanga unasema kuwa Morrison ana kandarasi ya miaka miwili huku mchezaji mwenyewe akieleza kuwa ana mkataba wa miezi sita ambao unameguka msimu utakapoisha.

Habari zinaeleza kuwa wakati wachezaji wakiwa kambini huku ulinzi ukiwa ni mkali Morrison alimua kusepa na alipobanwa aliwazidi ujanja walinzi na kusepa zake kuendelea na mipango yake mingine.

 Morrison ametupia jumla ya mabao matatu na ana pasi tatu ndani ya ligi huku kwenye Kombe la Shirikisho akiwa ametupia bao moja.

Post a Comment

0 Comments