BETI NASI UTAJIRIKE

MKATA UMEME AFUNGUKA BAADA YA KUIFUNGA YANGA


Kiungo mkabaji raia wa Brazil, Gerson Fraga amesema alijisikia furaha kubwa baada ya kufunga bao la kwanza katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Yanga uliopigwa juzi Jumapili Uwanja wa Taifa. Amesema baada ya kufunga bao lile dakika ya 21 alisubiri sekunde kadhaa kabla ya kuanza kushangalia akisikiliza kelele za furaha kutoka kwa mashabiki. Fraga ambaye ameingia kwenye kikosi cha kwanza kutokana na kiwango chake kuongezeka maradufu amekiri kuwa amewahi kushuhudia mechi za Derby nchini kwao Brazil lakini hii ya Bongo ni tofauti kutokana na hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki. "Ilikuwa furaha sana kwangu kufunga kwenye Derby kubwa kama hii, lilikuwa ni jambo la kipekee. Nilisubiri kwa sekundu mbili mpaka tatu kusikiliza kelele za mashabiki kabla ya kuanza kushangilia. "Mashabiki wanachangia kuongeza hamasa ya Derby kiukweli nimefarijika na nimefurahi sana na ninaomba waendelee kutupa sapoti," amesema Fraga. Kuhusu jina la 'Mkata Umeme' analoitwa na mashabiki Fraga amesema analifurahia kwa kuwa ni kawaida kwa wachezaji na wanaona mchango wake anaotoa kwa ajili ya timu. "Kwenye mpira ni kawaida kwa mchezaji kupewa jina na mashabiki kutokana na uchezaji wako hata mimi nalifurahia jina la Mkata Umeme kwa sababu linaonyesha thamani yangu ndani ya timu," amesema Fraga. Baada ya mapumziko ya siku mbili waliyopewa wachezaji na Kocha Sven Vandenbroeck kikosi kitaingia kambini usiku wa leo kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC utakaopigwa kesho kutwa Alhamisi.

Post a Comment

0 Comments