BETI NASI UTAJIRIKE

MENEJA SIMBA AFUNGUKA HALI YA SHOMARI KAPOMBE


Beki wa kulia wa Klabu ya Simba Shomari Kapombe inaelezwa kuwa kuna hatihati ya kukosa mechi zote za Simba msimu huu kutokana na majeraha ya mguu aliyopata.Kapombe aliumia mguu Julai Mosi Uwanja wa Taifa baada ya kuchezewa rafu na Frank Domayo nyota wa Azam FC.

Kwenye mchezo huo, wa hatua ya robo fainali Simba ilishinda mabao 2-0 watupiaji wakiwa ni John Bocco na Clatous Chama. 

Simba itakutana na Yanga Julai 12 Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa nusu fainali inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa Kapombe ataukosa pia mchezo huo. 

Mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Sahare All Stars na Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani.

Simba Julai 8 itamenyana na Namungo Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo watakabidhiwa kombe lao.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa wachezaji wote wa Simba wapo kambini isipokuwa Kapombe ambaye anaendelea kupewa matibabu. 
Kapombe ana jumla ya asisti saba ambapo ametoa sita Kwenye ligi na moja Kwenye Kombe la Shirikisho.

Post a Comment

0 Comments