BETI NASI UTAJIRIKE

MECHI RIPOTI:CHELSEA ILIVYOPIGWA 5 NA KUPOROMOKA MSIMAMO WA LIGI EPL


Klabu ya Chelsea imejikuta ikikubali kipigo cha 11 msimu huu wa 2019/20 baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-3 dhidi ya Liverpool mchezo uliopigwa dimba la Anfield. Naby Keita alikuwa wa kwanza kufungua nyavu za Chelsea dakika ya 23 huku Alexander Anold akifunga bao la pili dakika ya 38 Wiljnadamu akifunga bao la tatu dakika ya 43 .Oliivier Giroud alifunga bao la kwanza kwa Chelsea dakika ya 45+3 na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko Liverpool wakiwa mbele kwa mabao 3-1

Robert Firmino aliifungia Liverpool bao la 4 dakika ya 55 lakini Tammy Abraham alifunga bao la pili kwa Chelsea dakika ya 61 na Pulisic dakika ya 73. Ni Chamberlain aliyehitimisha ushindi kwa Liverpool baada ya kufunga bao la 5 dakika ya 84 na kuufanya mchezo huo mkali kumalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao 5-3 wakifikisha pointi 96 kwenye michezo 37 waliyocheza msimu huu.

Chelsea wameporomoka mpaka nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi na kuipisha Manchester United iliyotoka suluhu ya mabao 1-1 dhidi ya Westham United.Mnchester United na Chelsea zimefungana kwa pointi zote zikiwa na pointi 63 ila Manchester United wanamabao 13 zaidi ya Chelsea.

Chelsea wanatakiwa washinde mchezo wao wa mwisho dhidi ya Wolves kama watahitaji kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2020/21.

Post a Comment

0 Comments