BETI NASI UTAJIRIKE

MECHI RIPOTI: MASON GREENWOOD AIREJESHA MANCHESTER UNITED TOP 4 EPL


Mshambuliaji kinda wa Manchester United Mason Greenwood ameibuka shujaa kwenye mchezo dhidi ya Westham United uliomalizika kwa sare ya mabao 1-1. Westham walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Michael Antonio dakika ya 45+3 lakini   Greenwood alisawazisha bao hilo dakika ya 51 na kuufanya mchezo kumalizika kwa sare ya mabao 1-1.

Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kufikisha pointi 63 kwenye michezo 37 waliycheza msimu huu ikitua nafasi ya 3 baada ya kuizidi Chelsea kwa mabao 13 ya kufunga huku timu hizo zikilingana kwa pointi

Manchester United ina mchezo mgumu dhidi ya Leicester City iliyopo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 62 na kama mchezo huo watashinda au kutoa sare basi watashiriki Champions league msimu wa 2020/20

Post a Comment

0 Comments