BETI NASI UTAJIRIKE

MASAU BWIRE AFUNGUKA MAZITO KWA MASHABIKI WA SIMBA ,EYMAEL NA YANGA

Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting Masau Bwire ameskitishwa na baadhi ya mashabiki wanaotumia kauli za Luc Eymael kuwatania wenzao.Msemaji huyo amesema kitendo au kauli alizoongea kocha wa zamani wa Yanga ni za kulaani na sio kuzitumia kama utani. Akiongea kwa uchungu kwenye kipindi cha radio amesema, hajui kwa sasa kocha huyo (Eymael) yuko wapi
"Mpaka sasa vyombo vya usalama nchini vilitakiwa viwe vimemfukuza Tanzania ni mesikitishwa sana na baadhi ya mashabiki wanaofikia hatua ya kusema kuwa kama wao ni Simba kunatatizo gani kwa Yanga kuwa Nyani kwani wote ni wanyama. kauli hizo ni za kibaguzi na hazifai kutumiwa kama utani. Kwani waliutukanwa sio Yanga pekee bali ni nchi nzima ya Tanzania, mataifa Mengine nje hayajui kuwa ni Yanga ndio walioitwa NYANI bali wanajua ni Watanzania ndio waliobaguliwa kwa kuitwa jina hilo.

Post a Comment

0 Comments