BETI NASI UTAJIRIKE

MANCHESTER UNITED NI MWENDO WA DOZI TU,BRUNO FERNANDES MOTO MWINGINE


Klabu ya Manchester United imeendeleza ubabe ligi kuu Uingereza baada ya kutopoteza mchezo wowote tangu kurejea dimbani mwezi June.Manchester United imecheza michezo mitatu ya ligi huku ikishinda 2 na sare 1. Mbali na matokeo hayo klabu hiyo ilifanikiwa kuingia nusu fainali za FA kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Norwich.

Bruno Fernandes ameendelea kuonyesha uwezo wake baada ya kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Brighton.  Mshambuaji kinda wa klabu hiyo Green wood alikuwa wa kwanza kufunga dakika ya 16 Bruno akifunga dakika ya 29 na 50

Matokeo hayo yanaifanya Manchester kusalia nafasi ya 5 wakiwa na pointi 52 nyuma ya Chelsea wenye pointi 54 lakini wakiwa na mchezo dhidi ya Westham hii leo usiku

Post a Comment

0 Comments