BETI NASI UTAJIRIKE

MANCHESTER CITY YAWEKA REKODI MPYA STERLING AKIFUNGA HAT TRICK


Klabu ya Manchester City imeendelea kuimarika licha ya kupoteza ubingwa wa ligi kuu Uingereza msimu wa 2019/20. Hapo jana kwenye mcheo wa ligi kuu ikiwa ugenini iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Brighton . Huu unakuwa mchezo wa pili mfululizo kwa klabu hiyo kushinda mabao 5 baada ya kuiadhibu New Castle United mabao 5-0 siku chache zilizopita  na kuifanya klabu hiyo kuchez michezo 2 na kufunga mabao 10.

Kwenye mchezo dhidi ya Brighton vijana wa Guardiola walianza kupata bao la uongoza kupitia Raheem Sterling dakika ya 21 ,53 na 81 huku mabao mengine yakifungwa na Jesus dakika ya 44 na mreno Bernado Silva dakika ya 53.

Msimu huu Raheem Sterling ndiye mchezaji pekee kufunga hat trick mbili EPL akifanya hivyo dhidi ya Westham na Brighton. Bernado Silva ni mchezaji mwingine wa Manchester kufunga Hat trick msimu huu na aliifunga Watford kwenye mchezo walioshinda mabao 8-0.Aguero anaingia kwenye orodha akiwa na Hat trick 1 dhidi ya Aston Villa kwenye mchezo walioshinda 6-1

Kwa ushindi huo Manchester City inaendelea kukaa nafasi ya pili ikiwa na pointi 72 baada ya kucheza michezo 35 ikisaliwa na michezo mitatu tu kumaliza ligi kuu Uingereza.


Post a Comment

0 Comments