Msemaji wa klabu ya Simba bwana Haji Manara amefunguka ishu nzima kuhusu Frank Domayo na Shomari kapombe kwamba hakuna ugomvi kati ya wachezaji hao. Kapombe alitolewa nje ya uwanja baada ya kukanyagwa na Frank Domayo kwenye mchezo wa robo fainali kati ya Azam na Simba mchdzo uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 . Kupitia mitandao ya kijamii Manara aliandika Nimeongea na Frank @domayo na nimeongea na @shomari_12_kapombe , wenyewe wameyamaliza na @domayo kamuomba radhi Shomari na pia kampigia captain @john_22_bocco amuombee radhi kwa wachezaji wote wa Simba.
Sometimes mambo haya hutokea ktk football, tempo za uwanjani unaweza kufanya jambo usilolitegemea, hawa ni wachezaji marafiki na wameshamaliza.
Sasa niwaombe Wanasimba, cc ni klabu ya waungwana, tuna Washabiki wastaarabu na waelewa sana, nawasihi na kuwaomba Chonde Chonde msimtukane mitandaoni Domayo wala msimuone adui, tukimsamehe na cc Mungu atatusamehe makosa yetu.
Najua mnaniamini na mnafahamu jinsi nnavyoguswa na wachezaji wetu ktk matukio kama hayo, Pls Pls tusonge mbele, muhimu na la kushukuru Mungu hali ya @shomari_12_kapombe inaendelea vema 🙏🏾
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments