BETI NASI UTAJIRIKE

MAKALA: KIPI KIMEMKWAMISHA AJIBU NDANI YA SIMBA


Ibrahim Ajibu kiungo mshambuliaji ndani ya Simba kwa msimu wa 2019/20 ndio basi tena ndani ya kikosi hicho kuweza kuvunja rekodi yake aliyoweka msimu wa
2018/19 alipokuwa Yanga kwa kutoa jumla ya pasi 17 na kufunga mabao sita.

Mambo yamekuwa magumu ndani ya Simba kwa kuwaameshindwa kuonyesha makeke yake kutokana na kutokuwa na namba kikosi cha kwanza kinachonolewa na Sven Vandenbroeck.

Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 38 na kutwaa ubingwa wa ligi kwa msimu wa 2019/20 amecheza jumla ya mechi 19 akitumia dakika 1,154 amefunga bao moja na kutoa pasi tano za mabao kati ya 69.

Ana deni la mabao matano na pasi 12 ili aweze kuivunja rekodi yake aliyoiweka msimu uliopita ambapo haitawezekana tena kutokea kwa msimu huu wa 2019/20 kwa kuwa tayari umeshameguka mazima.

Mechi alizocheza ndan ya Simba:-JKT Tanzania(13),Kagera Sugar (90),Biashara United (77), Azam FC (6),Mwadui FC (30),Mbeya City (80), Tanzania Prisons (55), KMC (63),Ndanda (90), RuvuShooting (15),Mbao FC (85), Alliance (90), Namungo (56),Coastal Union (63),Polisi Tanzania (45),JKT Tanzania (90)Tanzania Prisons (45), Namungo,(71) na Mbao,(90).

Post a Comment

0 Comments