BETI NASI UTAJIRIKE

MAKALA: HENDERSON HAKUSTAHILI KUTWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA


Jordan Henderson ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu Uingereza msimu wa 2019/20 . Binafsi naona tuzo hizi zimetolewa kibaguzi kwani mchezaji huyo hajafanya lolote kubwa zaidi ya Sadio Mane, Mo Salah ,Van Dijk na hata aliyestahili tuzo hiyo Kelvin De Bruyne . Nimekuja na hoja tatu kubwa zinazotufanya tuamini tuzo hizo zimehujumiwa naFA (chama cha soka uingereza) ,wadhamini  wa tuzo Willam Hill na  hata waandishi,makocha na makapteni waliopiga kura za kumchagua mchezaji huyo.

1. Je Kimetumika kigezo cha usaidizi wa timu 

 Kelvin De Bruyne amehusika  kwenye mabao 31 kati ya mabao 102 yaliyofungwa na Manchester City msimu huu. De Bruyne amefunga mabao 11 na kutengeneza mengine 20 na hiyo ndiyo ilimfanya akaongoza orodha ya wachezaji waliotengeneza mabao mengi zaidi msimu huu. Trent Anord ametengeneza mabao 13  Andrew Robertson ametengeneza nafasi 12 Mohammed Salah ametengeneza nafasi 10 huku akifunga mabao 19. Hata ukiweka idadi ya wachezaji 10 huwezi kumuona Henderson kwenye orodha hii. Swali ni kipi kimemfanya Henderson ampiku De Bruyne.

2.  Ni Unahodha au Uraia wa kiingereza kilikuwa kigezo?

Nilimsikia mchambuzi mmoja wa kiingereza akisema Henderson anastahili kutwaa tuzo ya uchezaji bora kwani ameisaidia Liverpool kutwaa kombe la EPL kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30. binafsi hichi si kigezo sema tu waingereza walijiuliza mara mbili mbili iwaje tuzo ya mchezaji bora iende kwa wachezaji wa kibeligiji tena kwa mara mbili mfululizo?  msimu wa 2018/19 Van dijk raia wa Ubelgiji alitwaa tuzo hiyo Liverpool ikimaliza nafasi ya pili lakini msimu huu Manchester City imemaliza nafasi ya pili na raia wa Ubelgiji De Bruyne amemfunika kila kitu muingereza na nahodha msaidizi Henderson. Wayne Rooney raia wa uingereza alitwaa tuzo hiyo msimu wa 2009/2010 Ukichunguza kwa makini utagundua kwamba ndani ya miaka 10 mfululizo hakuna mchezaji yeyote wa Uingereza aliyewahi kutwaa  tuzo ya PFA . Kwa maana hiyo waingereza wameona waifiche aibu yao kwa Henderson.

3. Kimetumika kigezo cha kutwaa kombe la EPL?

Gareth Bale ametwaa tuzo hizo mara mbili bila Tottenham kutwaa kombe hilo,Robin Van Persie ,Luis Suarez ,Mo Salah na Van Dijk walitwaa tuzo hiyo bila kutwaa kombe lolote. Kombe si kigezo cha Henderson kutwaa tuzo hiyo. Hata wachezaji wa zamani wa Liverpool kama Jamie Carragher wamesema tuzo hizo zilifaa ziende kwa aidha Kelvin De Bruyne au Van Dijk. 

NB: Mwanzoni mwa msimu wa 2019/20 Henderson alikuwa anacheza box to box mid fielder lakini alibadilishwa nafasi yake baada ya kiungo fabinho kuumia hivyo alikabidhiwa mikoba ya kuwa namba 6 na kwa hakika aliimudu kisawasawa akicheza michezo 10 mfululizo na kwa umakini mkubwa huku Liverpool ikishinda michezo yote na kufungwa mabao matatu pekee. Nadhani kilitumika kigezo kilichotumiwa msimu wa mwaka 2016/17 kumpata Ngolo Kante 

Hitimisho :Mimi binafsi naona tuzo hizi zilihujumiwa kulinda heshima ya Taifa la Uingereza iliyopotea kwa miaka 10 mfululizo huku wachezaji wa kigeni wakitwaa tuzo hizo kwa kubadilishana

Post a Comment

0 Comments