BETI NASI UTAJIRIKE

MABIGWA WA NCHI WANAJAMBO LAO PALE UWANJA WA NDEGE NA MSIMBAZI


Klabu ya Simba imewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza uwanja w ndege jijini Dar es Salaam ili kuipokea klabu hiyo iliyotwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo.Sherehe za kuipokea timu hiyo zitaanzia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na sherehe hizo zitahamia mitaa ya msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaam.

Uongozi wa klabu umewaomba mashabiki wa klabu hiyo kufika uwanjani hapo majira ya saa mbili kamili asubuhi kuweza kuwapokea mabingwa hao mara tatu mfululizo.Wachezaji wa Simba watafika saa mbili na dakika 45 wakitokea mkoani mtwara wakiwa na kikombe cha ligi kuu Tanzania Bara.

Klabu hiyo inajiandaa kwa mchezo mwingine wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Yanga mchezo utakaopigwa tarehe 12 Julai siku ya jumapili jijini Dar es salaam.

Post a Comment

0 Comments