BETI NASI UTAJIRIKE

LIPULI ,PRISONS ZAPIGWA ,COASTAL UNION YATAMBA UGENINI
Alliance FC Mwanza imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Lipuli FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.Pongezi kwa wafungaji wa mabao hayo, David Richard dakika ya 34 na Sameer Vincent dakika ya 64 na kwa ushindi huo, Alliance FC wanafikisha pointi 40 baada ya kucheza mechi 34 na kupanda kwa nafasi tatu hadi ya 16.

Hali ni mbaya kwa Lipuli FC ikibaki na pointi zake 37 baada ya kucheza mechi 34 katika nafasi ya 17 – maana yake ipo hatarini kuipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu.

Nayo Coastal Union imewachapa 2-1 wenyeji, Tanzania Prisons kwenye mchezo mwingine wa Ligi Kuu Uwanja wa Sokoine. 

Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Shaaban Hamisi dakika ya 44 na Hamisi Kanduru dakika ya 49, wakati la Prisons limefungwa na Cleophace Mkandala dakika 90 na ushei kwa penalti.  


Coastal Union inapanda nafasi ya tano ikifikisha pointi 51 katika mchezo wa 34, wakati Tanzania Prisons inabaki nafasi ya 10 na pointi zake 44 za mechi 34.

Post a Comment

0 Comments