BETI NASI UTAJIRIKE

KWA SIMBA HII YANGA WAJIPANGE HIYO NUSU FAINALISimba na Yanga SC watakutana katika Nusu Fainali ya Kombe la Shiriksho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup baadaye mwezi huu.Hiyo ni baada ya Wekundu wa Msimbazi kufanikiwa kuitoa Azam FC kwa kuichapa mabao 2-0 katika mchezo wa mwisho wa Robo Fanali usiku wa leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mbali na Simba SC kumenyana na Yanga SC walioitoa Kagera Sugar ya Bukoba jana kwa kuwachapa 2-1 jana Uwanja wa Taifa pia - Sahare All Stars itamenyana na Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi iliyoitoa Alliance FC ya Mwanza jana kwa kuichapa 2-0.


Nahodha John Raphael Bocco aliifungia Azam FC bao la kwanza dakika ya 39 kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya kiungo Mkenya, Francis Kahata Nyambura kutokamupande wa kushoto.

Clatous Chota Chama akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 56 akimalizia pasi ya beki Shomari Salum Kapombe kutoka upande wa kulia.


Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’/Gardiel Michael dk88, Kennedy Juma/Erasto Nyoni dk46, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Gerson Fraga ‘Viera’,
 Clatous Chama, John Bocco, Luis Miquissone na Francs Kahata.

Azam FC; Benedict Haule, Nico Wadada, Salmin Hoza, Oscar Maasai, Abdallah Kheri, Mudathir Yahya/Bryson Raphael dk46, Bruce Kangwa/Iddi Kipagwile dk68, Frank Domayo, Richard Ella D’jodi, Never Tegere/Andrew Simchimba dk64 na Obrey Chirwa/Shaaban Iddi Chilunda dk76.

Post a Comment

0 Comments