Ligi kuu Uingereza imeendelea hapo jana kwa mechi kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali. Mechi iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu kabisa ni ile ya Aston Villa dhidi ya Arsenal mchezo uliopigwa dimba la Villa Park huku kiungo Trezeguet akiibuka shujaa kwa kurudisha matumaini ya AstonVilla kutoshuka daraja kwa pekee na maridadi kabisa dakika 27 ya mchezo. Bao la Trezeguet liliifanya Astonvilla kufikisha pointi 34 na kupanda mpaka nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 37 msimu huu huku wakibakiwa na mchezo mmoja muhimu zaidi dhidi ya westham. Hesabu za Astonvilla zilivyokaa Aston Villa yupo nafasi ya 17 na Watford yupo nafasi ya 18 wamefungana kwa pointi huku wote wakiwa na pointi 34 na wametofautiana kwa goli 1.Bournemouth wanapointi 31 na wako nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi. kwa maana hiyo kama Watford atashinda dhidi ya Arsenal atafikisha point 37 na kupanda mpaka nafasi ya 17 AstonVilla atapambana na Westham na kama atashinda mchezo huo basi atafikisha pointi 37 na kuwafanya wabaki nafasi ya 17 hivyo kutoshuka daraja msimu huu. AstonVilla ni lazima ashinde mchezo dhidi ya Westham ili aendelee kubaki EPL lakini pia Watfrod anatakiwa ashinde mchezo dhidi ya Arsenal ili asubirie matokeo ya Aston Villa kama Yeyote kati ya Aston villa au watford atafungwa kwenye mchezo wake wa mwisho basi atashuka daraja moja kwa moja na kama timu zote zitashinda mchezo wao basi tofauti ya magoli baina ya timu hizo mbili itaangaliwa. Vipi kuhusu Bournemouth? Timu hii ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 31. wanamchezo mgumu dhidi ya Everton na wanatakiwa kushinda mchezo huo . Sare au kufungwa kutawafanya kushuka daraja moja kwa moja . Ushindi dhidi ya Everton utawafanya wafikishe pointi 34 hivyo kuongeza ushindani kwa Aston Villa na Watfrod na kama timu hizo zitapoteza mchezo wao wa mwisho basi zitashuka daraja huku Watford akibaki nafasi ya 17.
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments