BETI NASI UTAJIRIKE

KUELEKEA DAR DERBY: HATUWEZI KUFUNGWA MECHI MBILI MFULULIZO NA YANGA

MSemaji wa Simba Haji Manara amefunguka kuelekea mchezo wa FA dhidi ya watani wao wa jadi Yanga. Manara amefurahishwa na klabu hizo kukutana kwenye mchezo huo wa nusu fainali na anaamini ni wakati sahihi kwa Simba kulipiza kisasi baada ya kupoteza mchezo wa Machi 8 kwa goli lililofungwa na Morrison. Manara alifunguka na kusema
Haitatokea, haitatokea Simba kufungwa mara mbili na klabu yoyote.Sio swala la kisasi unajua sisi lengo letu ilikua ni kuchukua double, ubingwa wa ligi kuu na FA.Kwani sisi Azam tulikuwa na ugomvi nao? Tungeweza kuwafunga hata sita lakini wachezaji wameheshimu wachezaji wenzao ile fedheha kumfunga mwenzako kwenye mechi kubwa kama ile goli tano au sita.Lakini kwa hawa, kwanza tutawalipia kisasi Kagera cha ule udhalimu wa juzi tutawalipia sisi.Kagera ni ndugu zetu wala msiwe na wasiwasi, si wametaka nusu fainali? Basi tukutane hiyo tarehe.
Lakini niwaambie mipango yao waliyopanga tarehe 8 safari hii itagonga mwamba, afe kipa afe beki Simba hawezi kufungwa mara mbili na Yanga

Post a Comment

0 Comments