Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ameweka wazi kuwa mchezo wa nusu fainali ya FA dhidi ya Yanga SC wanahitaji ushindi ili kutunza heshima ya klabu hiyo.Manara amesema baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wetu wa ligi kwa mara ya tatu mfululizo furaha itakuwa maradufu kama wataifunga Yanga na kuingia fainali ya FA siku ya Jumapili.
"Baada ya kupoteza mchezo uliopita tuliopokutana haitaleta picha nzuri mbele ya mashabiki wetu kama hatutapata ushindi na kutolewa
"Kuhusu hali ya wachezaji hilo msitie shaka wako na wameupa umuhimu mkubwa mchezo huu," amesema Manara.
Manara amesema amezungumza na mchezaji mmoja mmoja kuhusu umuhimu wa ushindi katika mchezo huu na wameahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wanawapa furaha Wanasimba.
"Tunafahamu mpira una matokeo matatu lakini Jumapili tunahitaji moja tu ambalo ni ushindi. Hatutakuwa na la kujitetea kama tutapoteza dhidi yao," amesema Manara.
Manara pia ameiomba Bodi ya Ligi kupanga waamuzi ambao watafuata sheria 17 za mpira na ikiwezekana wawe watano ili apatikane mshindi kwa haki.
0 Comments