BETI NASI UTAJIRIKE

KAULI MBILI ZA HAJI MANARA ZINAASHIRIA MSHIKAMANO KWA SOKA LETU


Afisa habari wa klabu ya Simba SC Haji Sunday Manara hapo jana alitoa ya moyoni baada ya kusambaa kwa sauti ya aliyekuwa kocha wa Yanga Lucy Eymael akitoa kauli za kibaguzi kwa mashabiki wa timu hiyo. Kupitia mitandao yake ya kijamii  haji manara aliwataka viongozi wa Yanga kumshughulikia kocha huyo.Manara alinukuliwa akisema .

Huyu Mzungu hafai kuendelea kufanya kazi Tanzania, kama Yanga kwa ujinga wao watashindwa kumfukuza na TFF ikashindwa kuchukua hatua, Serikali imfukuze nchini, hawezi kuwafananisha mashabiki wao na Nyani au mbwa, kama Watanzania ndugu zetu ni Nyani, nn kilimleta Tanzania? Angebaki kwao walipo Washabiki binadaam,,,ningekuwa Minister wa home affairs,Asubuhi tu ningeshanyang’anya vibali vyote vya kuishi na kufanya kazi hapa,,,
Hana heshma na hastahili kuendelea kufanya kazi ktk taifa hili linalojali utu na hadhi ya binadaam bila ubaguz


Baada ya malalamiko hayo Klabu ya Yanga ilimfuta kazi kocha huyo na kumtaka aondoke mara moja huku shirikisho la soka nchini TFF limejipanga kumpeleka kocha huyo kamati ya nidhamu FIFA ili ikiwezekana apewe adhabu ama kufungiwa kupewa vibali vya ukocha ndani ya Tanzania.Baada ya adhabu hizo Manara alinukuliwa akisema 

Hongereni @yangasc kwa kuchukua hatua sahihi na kwa wakati, hamkubaguliwa peke yenu ni Watanzania wote,Kampuni yangu ya H&M iliyopo South Africa 🤪🤪🤪ilibidi iombe radhi kwa tangazo la kibiashara lilionyesha viashiria vya kiubaguzi, vp tumuache muhuni huyu Mpiga Disco!!
Ktk hili mmepatia Washindi wa Pili wa ligi kuu.,,Shida yenu ni uwanjani tu

Post a Comment

0 Comments