BETI NASI UTAJIRIKE

KAGERE AFICHUA SIRI ZINAZOIPA SIMBA JEURI LIGI KUU


Mshambuliaji hatari wa Simba amefunguka kinachoipa jeuri klabu ya Simba mpaka kutwaa ubingwa mapema kabla ya mechi kumalizika. Kagere anaongoza safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo akifunga mabao 19 huku akiwa mfungaji mwenye mabao mengi zaidi kwenye msimamo wa ligi. 
Kagere amefanya interview na kufunga kinachoifanya Simba kuonekana imara.
Mishahara inatoka kwa wakati hauwezi kua na stress hata ukifunga mkashinda mechi mnapata bonus hii inasaidia sanaMshahara ni muhimu inatoa hamasa ya ushindi mara kwa mara."Tukienda mikoani mara nyingi unaona tunaenda na ndege, unaona timu nyingine zinazokuja kucheza na Simba wanakuja na gari kutoka mbali masaa karibia kumi hii inamsababishia uchovu mchezaji kwa hiyo inakua ngumu kupata matokeo."
- Kuhusu ufungaji bora
"Kitu cha kwanza nashukuru Mungu, kwa sababu yote yanayotokea Mungu ndio anaesababisha, ukifanya kazi yoyote lazima umuweke Mungu mbele, mimi namshukuru Mungu kwamba msimu wa kwanza nikawa mfungaji bora, sasa hivi pia namshukuru tena japo sijui matokeo yatakuwaje lakini mambo yatakuwa mazuri na ninaweza kuwa mfungaji bora tena."-
Kuhusu wanaobeza kuhusu umri wake
"Kawaida miaka yote wanasemaga ni mzee ni babu lakini mimi hua sipendi kuongea kuhusu miaka, ukitaka kunipa miaka unayotaka iwe 40, 50 lakini cha muhimu nipo nasaidia timu, unaweza kusema huyu ni mdogo lakini hawezi kusaidia timu.Mimi sijali mtu akiongea kuhusu umri, sijali hata kidogo.
"Nitakuwepo na nitakua vilevile, wakisema ndio Mungu atazidi kunipa mafanikio anayonipa, asiyenipenda ndiyo ajue nitazidi kufanikiwa."

Post a Comment

0 Comments