BETI NASI UTAJIRIKE

KAGERA SUGAR ,MWADUI NA TANZANIA PRISONS ZAENDELEA KUPETA VPL


Klabu za Kagera Sugar ,Mwadui na Prisons zimeendelea kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi baada ya kuibuka na ushindi kwenye mechi zao zilizopigwa leo jumatano tarehe 22-07-2020

1)Singida United  vs Kagera Sugar

Jahazi la Singida limeendelea kuzama vyema baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Kagera Sugar . Kelvin Kongwe wa Kagera Sugar alikuwa wa kwanza kufungua nyavu za Singida United kwa bao lake dakika ya 4 lakini Stephen Sey wa Singida alisawazisha bao hilo dakika ya 46 huku Awese Awesu akiipa Kagera bao la ushindi dakika ya 52. 

Kwa matokeo Kagera Sugar inakuwa na pointi 52 na kushika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi .

2)KMC FC vs Tanzania Prisons

Klabu ya KMC imeshindwa kupata ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Tanzania Prisons.Ramadhan Ibata aliipa Prisons bao la ushindi dakika 75 ya mchezo na kuifanya klabu hiyo kufikisha pointi48 ikikamata nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi. KMC mambo yamezidi kuwa kombo baada ya kipigo hicho wamebaki na pointi 46 wakiwa nafasi ya 12

3.)Mwadui vs Biashara United 

Mwadui wakiwa mkoani Shinyanga wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United huku bao hilo lilifungwa dakika ya 90+4 na Mussa Chambenga . Bao hilo mimewasaidia Mwadui kufikisha 44 wakiwa nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi .Biashara United wanabaki nafasi ya 10 wakiwa na pointi 47 kwenye msimamo wa ligi

Post a Comment

0 Comments