BETI NASI UTAJIRIKE

JESHI LA SIMBA HALIPOI NA HALIBOI LIKO TAYARI KUWANYUKA NAMUNGO FC


Klabu ya Simba imeendelea na mazoezi makali kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo FC.Mchezo huo utachezwa dimba la Majaliwa Stadium siku ya jumatano majira ya saa 11 jioni. Simba watakabidhiwa ubingwa wao wa msimu wa 2019/20 huku Namungu wakipambana kushinda mechi hiyo ili waweze kupanda mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

Vijana wa Sven wameendelea na mazoezi makali kuelekea mchezo huo wakijipanga kufanya vyema kwenye mechi hiyo ya ligi kuu  ambayo haina umuhimu sana kama watapoteza au watashinda kwani wamekwisha twaa ubingwa wa msimu huu.

Tarehe 12 Simba atacheza na Yanga kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la FA maarufu kama Azam Federation Cup.Mchezo huo utapigwa dimba la taifa Dar es salaam. Namungo wao watkuwa Majariwa Stadium kupambana na Sahare All Stars kwenye  mchezo huo wa nusu fainali.

Wachezaji Simba wakiendelea na Mazoezi kueleea mechi na NamungoPost a Comment

0 Comments