BETI NASI UTAJIRIKE

JESHI LA NAMUNGO LAELEKEA TANGA KUIVAA SAHARE ALL STARS


Kikosi cha Namungo kilicho chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thierykulazimisha sare ya bila kufungana na Simba, leo kimeanza safari kuelekea Tanga kuifuata Sahare All Stars.
Namungo ilikubali kugawana pointi mojamoja na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majaliwa.

Baada ya mchezo huo jana Julai, 8 Simba ilikabidhiwa rasmi kombe na kufanya sherehe za ubingwa na leo tayari wameshatia timu Dar kuendelea na shangwe za ubingwa.

Kwenye mechi mbili ambazo Namungo imekutana na Simba imesepa na pointi moja huku ikiyeyusha tatu Uwanja wa Taifa ilipopoteza kwa kufungwa mabao 3-2.

Sare hiyo inaifanya Namungo kubaki nafasi ya nne ikiwa na pointi 60 huku Simba ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 61 zote zikiwa zimecheza mechi 34.

Mchezo wake dhidi ya Sahare All Stars inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ni wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa Julai 12, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo wa nusu fainali utakaowakutanisha Simba na Yanga Uwanja wa Taifa.

Mshindi wa fainali ya mchezo huo atapata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kipa namba mbili wa Namungo, Adam Oseja amesema kuwa wameanza kuwafuata wapinzani wao Sahare All Stars baada ya kumalizana na Simba.

Post a Comment

0 Comments