BETI NASI UTAJIRIKE

JE IHEFU NA GEITA GOLD ZINAWEZA KUPANDA LIGI KUU?


Klabu za Geita Gold na Ihefu FC leo zitakuwa na kazi kubwa kuhakikisha zinapata ushindi kwenye michezo ya play off dhidi ya Mbao FC na Mbeya City. kama zitashinda raundi  ya kwanza basi timu hizo zitakuwa zimejirahisishia njia kuelekea kupanda ligi kuu.

Geita Gold wakiwa nyumbani wataikaribisha Mbeya City mchezo utakaopigwa dimba la CCM Kirumba mkoani mwanza. Ushindi wa timu hii utaifanya iwe imara zaidi kwenye mchezo wa marudiano pale jijini mbeya.

Ihefu wakiwa nyumbani mbarali mkoani Mbeya watakuwa na kibarua kikubwa uhakikisha wanapata ushindi ili mambo yawe rahisi kwenye mchezo wa pili timu hizo zitakapokutana uwanja wa ccm kirumba mkoani Mwanza.

Post a Comment

0 Comments