BETI NASI UTAJIRIKE

HONGERENI DODOMA FC NA KARIBUNI SANA LIGI KUU TANZANIA BARA


Dodoma FC imefanikiwa kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Iringa United leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.Kwa matokeo hayo, Dodoma FC iliyo chini ya kocha Mbwana Makatta inamaliza kama kinara wa Kundi A kwa pointi zake 51 za mechi 22 ikiizidi wastani wa mabao tu Ihefu ambayo leo imeichapa Cosmopolitan 3-0.
Mechi za mwisho za Ligi Daraja la Kwanza 


, Boma FC imeichapa 3-0 Friends Rangers, Pan African imefungwa nyumbani 2-1 na Maji Maji FC, African Lyon imeichapa 4-2 Mlale FC na Njombe Mji FC imeshnda 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza.

Kwa matokeo hayo, Dodoma FC inaungana na Gwambina FC ya Misungwi mkoani Mwanza kutoka Kund B kupanda Ligi Kuu msimu ujao.
Ihefu FC ya Mbarali Mbeya na Maji Maji ya Songea mkoani Ruvuma kutoka kundi A zimefuzu kucheza michezo ya mchujo Play Off ya kupanda ligi kuu. Huku Geita Gold ya Geita na Trans Camp ya Dar zimefuzu kucheza play Off kutoka kundi B.

Mlale FC, Pan African, Cosmopolitan FC na Iringa United zimeshuka daraja la pili (SDL) kutoka kundi A huku Timu za Boma FC na Friend Rangers zitacheza play off ya kubaki ligi Daraja la kwanza au kushuka Daraja la Pili (SDL) kutoka kundi A

Green Warriors, Sahare All Stars, Stand United na Mawenzi Market FC zote zimeshuka daraja kwenda daraja la Pili  (SDL) kutoka kundi B huku Mashujaa na  Pamba/Arusha FC zitacheza play off ya kubaki daraja la kwanza au kushuka Daraja la Pili kutoka kundi B.

Post a Comment

0 Comments