BETI NASI UTAJIRIKE

HIKI NDICHO CHANZO CHA DODOMA FC KUKAMULIWA FEDHA NA TFF


Dodoma FC imepigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000) kwa kosa la kugoma kuingia vyumbani baada ya kukuta yai limepasuliwa mbele ya lango la kuingilia katika chumba chao cha kubadilishia.

Kugoma kwao kulisababisha zoezi la ukaguzi wa wachezaji lifanyike nje ya chumba katika mchezo uliochezwa Juni 27, 2020 mkoani Ruvuma.

Adhabu hii imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za mchezo.
Mchezo huo ulikamilika kwa Majimaji kufungwa mabao 2-1 mbele ya Dodoma FC.

Pia Kiongozi wa timu ya Ruvuma Queens Bw. Issa Telela amepelekwa kamati ya nidhamu ya TFF kwa kosa la kumtemea mate mwamuzi wa akiba katika mchezo uliochezwa Juni 27, 2020 kwenye uwanja wa Sokoine Mkoani Ruvuma.

Post a Comment

0 Comments