BETI NASI UTAJIRIKE

HATMA YA MBAO FC IPO MIKONONI MWA SIMBA HII LEO


Nahodha wa klabu ya Simba John Rafael Bocco amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa  dhidi ya Mbao FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa hii leoSimba leo walifanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Mo Simba Arena kwa ajili ya kumalizana na Mbao FC iliyo chini ya Felix Miziro.

Mchezo wao walipokutana mzunguko wa kwanza Uwanja wa Kirumba, Simba ilishinda mabao 2-1 na kusepa na pointi tatu mazima inakutana na Mbao FC ambayo inapambana kushuka daraja.

Ipo nafasi ya 19 ikiwa imejikusanyia pointi 35 baada ya kucheza 34 na inakutana na Simba ambao ni mabingwa wakiwa nafasi ya kwanza na pointi 81.
Mchezo uliopita Mbao ilishinda bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar inayonolewa na Zuber Katwila.

Bocco amesema:"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu na tunatambua kuwa utakuwa mgumu tutapambana mashabiki watupe sapoti."

Post a Comment

0 Comments