Klabu ya Yanga hii leo inacheza mchezo wake wa 37 Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro majira ya saa 10:00 jioni. Kuna uwezekano wachezaji wao nane wakaukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali ambazo zimeelezwa ikiwa ni pamoja na majeruhi pamoja na wale ambao hawapo kwenye mpango wa kocha. Nyota hao ni pamoja na:-Haruna Niyonzima anasumbuliwa na majeraha ya goti, Mapinduzi Balama yeye pia anasumbuliwa na majeraha aliyopata mazoezini, Papy Tshishimbi bado hajawa fiti. Ally Ally, Andrew Vincent, Eric Kabamba, Ramadhan Kabwili, Raphael Daud hawa hawapo kwenye mpango wa mwalimu, Luc Eymael hivyo iwapo atawatumia ni kwa muda mchache ndani ya kikosi cha leo. Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 68 inamenyana na Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 41 zote zimecheza mechi 36.
0 Comments