Klabu ya Simba imekubali kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Mbao kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara raundi ya 35. Mbao FC walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 5 lililowekwa kimiani na Rajabu Rashidi lakini Meddie Kagere alisawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penati ya dakika 35.Waziri Junior alirudi tena nyavuni kwa Simba na kuandika bao la pili dakika ya 45+2 na kufanya mchezo huo kwend mapumziko Simba wakiwa nyuma kwa mabao 2-1. Miraji Athumani aliisawazishia Simba bao la pili dakika ya 52 lakini Jordan John aliipa ushidi mbao kwa bao maridhawa dakika ya 59.Mpaka mpira unamalizika Mbao FC 3-2 Simba. Tathmini ya mchezo. Mchezo huo ulikuwa muhimu kwa mbao fc wasiweze kushuka daraja kama wangefungwa.Mbao FC wamefikisha pointi 38 baada ya kuifunga Simba na kuwafanya waendelee kutetea nafasi ya kubaki ligi kuu. Unaweza kusema Simba haikuwa na habari na mchezo huo kwani imeshatwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu na hilo linadhihirika baada ya kuchezesha kikosi cha wachezaji wa kawaida kabisa ambao msimu huu wengi wao hawajacheza mechi nying huku pi akiwapumzisha nyota wa kikosi cha kwanza kuelekea mchezo wa fainali dhidi ya Namungo FC mjini Sumbawanga. Kikosi cha Simba kiliongozwa na Ally Salim,Haruna Shamte,Gadiel Michael,Mlipili ,Nyoni,Said Hamis,Dilunga,Mzamiru,Kagere,Ajibu na Miraji Athuman
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments