BETI NASI UTAJIRIKE

EYMAEL ATOBOA SIRI INAYOIKWAMISHA USHINDI YANGA


Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anahofu kubwa juu ya Uwanja wa Karume atakautumia kesho watakapomenyana na Biashara United.
Yanga itawavaa Biashara United ikiwa na kumbukumbu ya kusepa na pointi tatu kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa kwa ushindi wa bao 1-0.
Eymael amesema kuwa anaamini mchezo utakuwa mgumu kutokana na ushindani uliopo pamoja na ubovu wa uwanja jambo litakaloongeza ugumu.
Viwanja vingi vya nje ya Dar ni vibovu na vibaya kwenye kutafuta matokeo, ninaamini mchezo wetu dhidi ya Biashara United ni Mungu mwenyewe anajua hali itakavyokuwa,” amesema Eymael.
Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 60 huku Biashara United ikiwa nafasi ya 9 na pointi 44 zote zimecheza jumla ya mechi 32 kwenye ligi.
Kwenye mechi yake mbele ya JKT Tanzania iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na ule dhidi ya Mwadui FC uliochezwa Kambarage, Eymael alisema kuwa matokeo mabovu aliyopata yalichangiwa na sehemu ya kuchezea.
Atakosa huduma ya kiungo wake Balama Mapinduzi mwenye mabao matatu na pasi moja ya bao ambaye anasumbuliwa na majeraha ya mguu aliumia kwenye mazoezi wakatu Yanga ikijiandaa kuivaa Ndanda FC.

Post a Comment

0 Comments