BETI NASI UTAJIRIKE

CHELSEA NI MWENDO WA KUPIGA TATU WAKIINGIA NAFASI YA TATU KIBABE


Klabu ya Chelsea imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Crystal Palace na kuwafanya kurejea nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na jumla ya pointi 60.Chelsea walikwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Olivier Giroud dakika 6 tu  ya mchezo Huku Pulisic akifunga bao la  pili dakika ya 27.Crystal Palce walirejea mchezoni baada ya Wilfred Zaha kufunga bao dakika ya 34 lakini Tammy Abraham akizima ndoto zao kwa bao la tatu dakika ya 71 huku Benteke akifunga bao la pili kwa Crystal Palce dakika ya 72 ya mchezo huo.

Mpaka mchezo unamalizika Chelsea walikuwa mbele kwa mabao 3 dhidi 2 ya Crystal palace. 

Kitendo cha Arsenal kutoka sare na Leicester City kimeipa faida Chelsea na kuifanya timu hiyo kubakiza pointi 6 kuweza kuikuta Manchester City aliye nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi akiwa na pointi 66 baada ya michezo 33

Post a Comment

0 Comments