BETI NASI UTAJIRIKE

BIASHARA UNITED WATANGAZA VITA NA RUVU SHOOTING BAADA YA SARE NA YANGA


Kocha Mkuu wa  Biashara United Francis Baraza amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kusaka ushindi mbele ya Ruvu Shooting. Mchezo huo utachezwa leo Uwanja wa Karume ambapo akishinda ama kulazimisha sare atafikisha jumla ya mechi 10 bila kufungwa Uwanja wa Karume.

Mchezo wake uliopita ililazimisha sare ya bila kufungana na Yanga ndani ya dakika 90, Julai 5 huku Ruvu Shooting nao wakitoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar,  Uwanja wa Kaitaba.

Baraza amesema:"Tupo tayari kupata matokeo mbele ya Ruvu Shooting tunawaheshimu wapinzani wetu ila tutakuwa nyumbani na mashabiki wetu pia.

"Rekodi ya kufikisha mechi 10 bila kufungwa ni jambo jema na imani yangu baada ya dakika 90 tutajua tupo wapi na tumefanya nini mashabiki wajitokeze kutupa sapoti, " amesema.

Post a Comment

0 Comments