advertise with us

ADVERTISE HERE

BEKI MPYA WA SIMBA KUMBE ANASIMAMIWA NA MENEJA MZUNGU


Taarifa rasmi imesema klabu ya Simba imefanikisha dili la kumnasa David  Kameta,'Duchu' beki wa Klabu ya Lipuli FC,Taarifa hiyo inaelezwa kuwa amesaini mkataba wa miaka miwili ndani ya Klabu ya Simba.

Beki huyo msimu huu amekuwa kwenye ubora wake ndani ya Lipuli ambapo amefunga mabao matatu na kutoa pasi saba za mabao.Sababu kubwa ya Kameta kuachana na Lipuli kwa msimu wa 2020/21 ni timu hiyo imeshuka daraja baada ya kufikisha pointi 44 ikiwa nafasi ya 18 hivyo msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Itakumbukwa beki huyo makini alikuwa anasimamiwa na Balozi wa Lipuli FC ya mkoani Iringa Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo

Post a Comment

0 Comments