BETI NASI UTAJIRIKE

BARCELONA WAVULIWA UBINGWA WAKICHEZEA KIPIGO NOU CAMP


Klabu ya Barcelona imekubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Osasuna mchezo uliopigwa dimba la Nou Camp. Osasuna walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 15 lililowekwa kimiani na Jose Arnaiz .Lionel Messi alisawazisha bao hilo dakika ya 62 lakini Roberto Torres aliipa Osasuna bao la ushindi dakika  ya 90 +4 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Osasuna 2-1 Barcelona.

Matokeo hayo yameifanya Real Madrid kutwaa rasmi La Liga msimu wa 2019/20 wakifikisha pointi 86 na kuwaacha Barcelona kwa pointi 7 baada ya timu zote kucheza michezo 37.

Lionel Messi anaongoza Orodha ya wafungaji bora La Liga akiwa na mabao 23 huku anayemfuatia ni Karim Benzema mwenye mabao 27.

Post a Comment

0 Comments