BETI NASI UTAJIRIKE

BAADA YA KUMTIMUA EYMAEL YANGA WAZIDI KUTETELEKA
Kaimu katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick amesema Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ameomba kupumzika kukinoa kikosi hicho.

Mkwassa alikuwa anafanya kazi na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Luc Eymael ambaye amefutwa kazi.

Eymael alifutwa kazi ndani ya Yanga, Julai 27 baada ya kueneza taarifa zilizokuwa na viashiria vya ubaguzi wa rangi jambo ambalo sio la kiungwana kwa familia ya michezo na dunia nzima kiujumla.

 Katibu amesema kuwa Mkwassa kwa sasa ameomba kupumzika na majukumu ya kukinoa kikosi hicho hivyo watalazimika kumtafuta mbadala wake 

Post a Comment

0 Comments