BETI NASI UTAJIRIKE

AZAM YAWAPOTEZEA MAZIMA NYOTA WAKE WATATU KIKOSI CHA KWANZA


Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' amesema kuwa wamewaacha nyota 

wao watatu ndani ya kikosi hicho ikiwa ni mpango wa kufanya maboresho ndani ya kikosi 

hicho.

Jana, Julai 30, Azam FC ilimtambulisha kiungo Awesu Awesu kwa dili la miaka miwili akiwa
 ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Kagera Sugar.

Popat amesema:-“Kwenye mapendekezo yake wapo nyota ambao tumeamua 

kuachana nao ikiwa ni pamoja na Donald Ngoma, Emmanuel Mvuyekure na Razack Abarola ambao mikataba yao imeisha.

"Yote tunayofanya ni mapendekezo ya kocha Arstica Cioaba ambaye anahitaji kuwa na 
kikosi bora msimu ujao, bado tunaendelea kuboresha kikosi kwa mapendekezo ya benchi la ufundi," amesema.

Awesu alikuwa kwenye rada za Yanga ambao wameikosa saini ya nyota huyo mwenye

 mabao saba kwenye mashindano yote ndani ya msimu wa 2019/20.

Aliwahi pia kukipiga ndani ya Azam FC wakati alipokuwa kwenye Academy ya Azam FC 

2014/15 kabla ya kuondoka na kuibukia Arusha.

Post a Comment

0 Comments